Tuesday, October 11, 2016

ICARDI AMJIBU MARADONA.




Mauro Icardi
Kumekuwa na maneno ya hapa na pale kutoka kwa Diego Maradona dhidi ya nahodha wa Inter Milan Mauro Icardi kwenye vyombo vya habari.
Baada ya nahodha huyo wa Inter Milan kufunga ndoa na aliyekuwa mke wa mchezaji mwenzake wa zamani katika timu ya Sampodoria Maxi Lopez, Wanda Nara, miezi michache baada ya wanandoa hao kutalikiana, na ndipo bingwa huyo Kombe la Dunia 1986 Maradona kuanza kumlipua mchezaji huyo juu ya suala hilo. 
 
Diego maradona.


June mwaka huu ambapo Maradona aliwaambia waandishi wa habari kwamba mshambuliaji huyo wa Argentina (Icardi) kwake ni kama mtu aliyekufa na kwenda mbali zaidi kwa kumuita msaliti, kitendo ambacho kimemfanya nahodha huyo wa Inter kumjibu mkongwe huyo.   

''Alikuwa mchezaji imara na bora, lakini nj'e ya soka siwezi kujibu chochote,'' Icardi aliiambia Sky Sport Italia. 

''Nadhani anavuka mipaka kama alivyofanya mwaka uliopita, na kwa mahojiano kama hayo ayawezi kuleta amani.   

''Hayo ni maneno yasiyo kuwa na maana, ilishatokea kwenye mchezo wa kirafiki uliopangwa na Javier Zanneti. Siwezi kuongea kitu chochote kwa mtu asiyekuwa mfano kwa yeyote.'' 

Icardi ambaye ameanza vyema msimu huu wa Serie A, akiwa na mabao sita katika mechi saba kwa Inter. 

No comments:

Post a Comment