Muingereza Kyle Edmund atakutana na mchezaji namba tatu duniani kwa ubora kwenye mchezo wa tenisi Stan Wawrinka kwenye hatua ya pili ya michuano ya Shanghai Masters baada ya kumfunga Federico Delbonis wa Argentina kwa seti 6-3 5-7 6-4.
Edmund ambaye amepanda kiwango na kuwa namba 48 katika viwango vya mchezo huo atakutana na Wawrinka ambaye amepania kujaribu kushinda taji hilo la Shanghai Masters kwa mara ya tano mwaka huu 2016.
No comments:
Post a Comment