![]() |
| Gerard Pique na Lionel Messi. |
Nyota wa Barcelona Gerard Pique anaamini athari zitakazotokea siku mchezaji mwenzake Lionel Messi atakapoachana na timu hiyo ya Nou Camp na kusema kwamba itakuwa kama ''ni siku ambayo baba yako anakufa.''
Messi ambaye ni zao la La Masia na amekuwa na maendeleo mazuri toka awe timu ya wakubwa kiasi cha kuwa mchezaji bora wa wakati wote klabuni hapo.
Pique ambaye alikuwa pamoja na Messi La Masia aliondoka na baadaye kurudi Barca, anajua athari za Messi siku akiondoka.
''Ni wa ajabu, siku atakayo ondoka itakuwa kama vile baba yako anakufa, na hilo litakuwa gumu sana kukubalika,'' aliiambia TV3.
''Tunaongea kuhusu Leo sasa, lakini siku moja hatakuwepo hapa na tutakuwa uchi, na tutaanza kuendelea kuwa kwenye ushindani.''
Messi ambaye ameshashinda taji la LaLiga mara 8 na Klabu ya Mabingwa mara 4 miongoni mwa mataji mengine Barca.
![]() |
| Busquet,Messi,Xavi na Iniesta. |
Pia Pique alisema kwamba hakutakuwa na kizazi kingine kama cha Messi, Xavi, Sergio Busquets, Carlos Puyol, Iniesta na yeye mwenyewe.
''Hakutakuwa na Messi mwingine, na hatutarajii hilo kuwepo kama ambavyo tusivyotarajia kuwepo kizazi kingine La Masia kama ,Xavi, Puyol, Busquet,Iniesta na mimi mwenyewe,'' Aliongezea.
''Acha tuendelee kujipa matumaini lakini sifikiri kama kitakuwepo tena.''


No comments:
Post a Comment