Tuesday, October 4, 2016

MARC OVERMANS AMPIGIA DEBE WENGER TIMU YA TAIFA ENGLAND

Image result for arsene wenger images



Marc Overmars amempigia debe Arsene Wenger kama mgombea atakae kuwa kocha ajaye kwa timu ya taifa ya Uingereza.
Kocha huyo wa Arsenal ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, baada ya aliye kuwa kocha wa timu hiyo Sam Allardyce,kuvunja mkataba baada ya kuitumikia kwa mechi moja , baada ya kuvuja kwa mahojiano yake na waandishi wa habari juu ya usajili wa wachezaji kinyume na taratibu. 

Overmars ambaye ni Mkurugenzi wa Ajax, alishinda Premier League  na FA akiwa chini ya Wenger, anaamini koch huyo mwenye miaka 66 anaweza kuwa kocha sahihi wa Uingereza. 

''Nazani atakuwa chaguo sahihi kwa Uingereza.'' mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi Overmas aliiambia ASPIRE4SPORT.  

''Labda ni muda wake, kama ana nguvu ya kuweza kufanya hivyo.'' 

Kwa sasa kocha wa Uingereza U-21 Gareth Southgate ndie amepewa majukumu ya kuiongoza timu hiyo kwa mechi nne zijazo huku FA wakiendelea kumtafuta mrithi wa Allardyce.  

No comments:

Post a Comment