Tuesday, October 11, 2016

IWOBU ANA MCHANGANYIKO WA OKOCHA NA DAVIDS- OZIL

Alex Iwobu kwenye moja ya majukuu yake akiwa Arsenal.
Nyota wa Arsenal Mesut Ozil amefurahishwa na kiwango cha mchezaji mwenzie wa klabu hiyo Alex Iwobu kiasi cha kumfananisha na mjomba wa mchezaji huyo Jay-Jay Okocha na nyota wa zamani wa Uholanzi Edgar Davids.
Iwobu amekuwa na maendeleo mazuri kwa Gunners toka awe anaanza kwenye kikosi hicho msimu uliopita huku Ozil akiwa hana na lakusema zaidi ya kumsifia winga huyo ambaye anawapa kile Arsenal wanahitaji kwenye eneo la winga. 
 
Ozil na Iwobu kwenye moja ya majukumu yao Arsenal. 

''Ananikumbusha juu ya mjomba wake Okocha,'' Ozil alisema kuwa mchzaji huo wa Arsenal ni mchezaji anaependa kumuangalia. Alex ananikumbusha mchanganyiko wake na Davids.   

''Ni imara kwenye mpira, pia anazuia, lakini ni mzuri mbele ya goli. Anajua jambo sahihi la kufanya.Hana woga na hajifichi uwanjani. 

''Anataka kucheza mpira kwa furaha na hilo analionyesha akiwapo uwanjani, na hata mazoezini. 

''Ana maendeleo mazuri na kama ataendelea hivi atacheza msimu wote, ataongeza kiwango chake kwenye michezo na kocha anajua ubora alionao na nina mtakia kila la kheri. Ni mdogo  na kwa kweli yuko kwenye njia nzuri.
 

No comments:

Post a Comment