![]() |
| Pepe |
Miamba ya Italia Juventus wameonyesha nia yao ya kutaka kumsajili beki wa Real Madrid Pepe ambaye mkataba wake na Los Blancos unatarajiwa kuisha June 2017 kwa mujibu wa Tottosport.
Bianconeri ambao wanafahamika kama wataalamu wa kuleta wachezaji kwa ajili ya kuimarisha timu yao kama walivyothibitisha kwa wachezaji Andre Pirlo, Sami Khedira na Dani Alves .
Na kuanzia January Mreno huyo atakuwa huru kujadili na klabu yoyote juu ya hatma yake ya soka.
Pepe ambaye anaonekana muhimili mzuri kwa Los Blancos kutokana na kazi ya udhibiti kwa wapinzani na kadhia anayowapa pindi wanapokutana nae anatarajia kuachana na miamba hiyo ya Hispania kama hakutakuwa na mazungumzo baina yao.

No comments:
Post a Comment