Baada ya hapo jana kupokea kipigo kutoka kwa Sundowns katika fainali ya ligi kuu barani Afika,Mwenyekiti wa Zamalek Mortada
Mansour amelaumu "uchawi na bahati mbaya" kwa kushindwa kwa timu yake
mikononi mwa timu ya Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns.
Mwenyekiti huyo amesema kwamba "kulikuwa na nafasi nyingi kwetu sisi
katika mechi zote, lakini mpira ulikataa kutingisha nyavu" Mansour
aliongeza, baada ya kushindwa mabao 3-1 kwa jumla ya mabao.
''Hivi inawezekana kweli hukose nafasi 18 mbele ya goli? mambo hayakuwa sawa kweli kulikuwa na nguvu za giza na uchawi.'' Aliongezea Mwenyekiti huyo.
Pia aliunga mkono kwa kocha Moamen Soliman kusalia katika nafasi yake licha ya kupoteza.
"Tuna wakufunzi wazuri na sitawafuta kazi," amesema Mansour, mbaye aliwatumia wakufunzi sita mwaka huu.
"Kocha Moamen atasalia kama mkufunzi mkuu wa Zamalek, hadi mwisho wa msimu huu."
Mabingwa hao wapya watacheza Kombe la Dunia la klabu nchini Japan.
Mafanikio ya Sundowns kuwa klabu yenye ushindani yamekuja miaka 21 baada ya klabu ya Orlando Pirates kuwa timu ya kwanza ya South Africa kushinda taji hilo.


No comments:
Post a Comment