Monday, October 24, 2016

BALLON D'OR YANOGA 30 KUTAJWA KUIWANIA.


Jumatatu hii orodha ya majina 30 ya wachezaji itatolewa kwa ajili ya tuzo ya Ballon d'Or 2016 huku Andre Iniest na Koke wakiwa Wahispania wa kwanza kuwania tuzo hiyo.Mshambuliaji wa timu ya Wales Gareth Bale na mwenzake wa Real Madrid Cristiano Ronaldo wameorodheshwa kuwania taji la mchezaji bora duniani mwaka 2016 Ballon d'Or.


Tuzo hiyo hutolewa na Ufaransa kila mwaka tangu mwaka 1956, lakini kwa kipindi cha miaka sita iliopita tuzo hiyo ilibadilika na kuwa Fifa Ballon d'Or kwa ushirikiano na shirikisho la soka duniani Fifa.Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita kwa mara ya tano . Na majina hayo yanatangazwa kufuatia herufi za jina la mchezaji.

Wachezaji wa Manchester City Sergio Aguerro na Kevin De Bruyne, pamoja na wachezaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann pia wako katika orodha hiyo.
Gazeti la soka la Ufaransa limebaini orodha ya wachezaji 30 katika makundi ya wachezaji watano kila baada ya saa mbili siku yote ya Jumatatu.
  • Wachezaji wengine waliorodheshwa ni pamoja na:
Sergio Aguero (Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Paulo Dybala (Juventus), Diego Godin (Atletico Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus).
 Riyad Mahrez, Marcelo, Leo Messi, Luka Modric, Thomas Mueller, Manuel Neuer, Neymar, Jan Oblak, Mesut Ozil, Dimitri Payet, Pepe, Gerard Pique, Paul Pogba, Renato Sanchez, Luis Suarez, Jamie Vardy na Arturo Vidal, Sergio Busquets, James Rodriguez na Alexis Sanchez

No comments:

Post a Comment