![]() |
| Sturridge akifunga moja ya mabao yake mawili hapo jana dhidi ya Houtspurs. |
Baad ya hapo jana mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge kuiwezesha timu yake kutoka kifua mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham Houtspurs na kuisaidia Liver kufikia hatua ya robo fainali ya Kombe la EFL kwenye uwanja wa Anflied hapo jana. Kocha wa Liver Jurgen Klopp amesema kwamba hakuwai kutilia shaka uwezo wa mshambuliaji huyo kwenye kikosi chake.
Klopp alisema hayo baada ya hapo jana Sturridge kufunga mabao mawili peke yake kwenye ushindi huo hapo jana nyumbani Anfield.
Magoli hayo yalikuwa ya kwanza kwa mchezaji huyo wa timu ya tifa ya Uingereza kwa klabu yake toka Agosti , hali ilimyofanya Klopp kusema kwamba hakuwahi kuhoji uwezo wa nyota huyo mwenye miaka 27.
''Hiko ni kipaji chake, hilo ni muhimili wake. Yeye ni mmaliziaji , ni mshambuliaji mzuri, hakuna mashaka kuhusu hilo,'' alisema Mjerumani huyo.
'Sikuwahi kuwa na mashaka juu ya hilo, hata pale ambapo hajafunga. Hakukuwa na maswali. Hatukujadili uwezo.''
''Divock Origi hakufunga bao usiku lakini amecheza vizuri. Danny Ings hakufunga bao alipoingia lakini amecheza vizuri sana.
''Daniel kufunga mabao safi kwetu, ni muhimu sana. Kwenye wakati muafaka , yeye na wachezaji wengine wanaweza kufunga , na hilo linaweza kuwa bora kwetu. Linaweza kuwa bora sana.

No comments:
Post a Comment