Wednesday, October 26, 2016

MOURINHO AOMBA RADHI MASHABIKI WA UNITED DUNIANI KOTE.


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amewaomba radhi wapenzi na mashabiki wa Man U duniani kote kufuatia kipigo walichopata Jumapili cha 4-0 dhidi ya Chelsea Stamford Birdges akisema kwamba ''hayakuwa matokeo ya United na wote wanaomba msamaha kwa hilo.''
 
United ambao wanaelekea mechi yao dhidi ya Manchester City kwenye kombe la Ligi siku ya leo, kocha huyo Mreno ameonyesha masikitiko yake kwa kilichotokea siku ya Jumapili Stamford Birdges.

Alielezea kwenye mipango yake mbele ya mechi yao dhidi ya City, Mourinho alianza kwa kuomba radhi kwa mashabiki, wapenzi na wadau wa United duniani kote.

Aliandika ''Kama kiongozi wa kikosi ningependa kuanza na samahani kwa mashabiki wote wa United duniani kote.

''Matokeo ya Jumapili hayakuwa matokeo kwa United, bali yametufanya wote tuombe radhi kwa wadau, wapenzi na mashabiki na wote tunaomba msamaha juu ya hilo. 

''Kwa mara nyingine tena mashabiki wetu Stamford Bridges walikuwa na huzuni, siwezi kufikiria idadi ya mashabiki ambao mpaka dakika 90 wanaimba na timu yao inapoteza. Wanakuwa wamejitolea kwa klabu ninajisikia kuwapa pole kwa yale matokeo ambayo hayakuweza kuendana na utendaji wao.

''Nina uhakika hata Manchester City pia hawako na furaha kwa muenendo wao walionao kwa sasa kwani wiki iliyopita nao walipoteza 4-0 dhidi ya Barcelona na leo wanacheza wakiwa na mfululizo wa kucheza mechi tano bila ushindi , lakini hilo halibadili kuwa ni timu nzuri, wana meneja mzuri na wachezaji wenye uzoefu.

Timu hizo mbili za jijini Manchester zote ziko kwenye hali mbaya baada ya wote kupokea vipigo vya 4-0 kwenye mechi zao muhimu na leo wanakutana kwenye Kombe la Ligi.

No comments:

Post a Comment