![]() |
| Luis Enrique, Kocha Mkuu Barcelona. |
Licha ya kuiongoza Barcelona kushinda taji la LaLiga msimu uliopita, kocha wa Barcelona hakuwepo kwenye idadi ya makocha watatu bora wa mwaka wa LaLiga na kocha huyo akatania kwamba anajiona yeye ni mmoja wa makocha 20 bora wa LaLiga. Enrique ambaye hakuwepo kwenye tatu bora kwenye tuzo hizo ambazo kocha wa Atletico Madrid Dieogo Simeone alishinda tuzo hiyo.
Akiulizwa kuhusu kutokuwepo kwake kwenye tatu bora hiyo, kocha huyo raia wa Australia mwenye miaka 46 akatania kwamba yeye ni mmoja wa makocha bora wa LaLiga.
''Hilo ni swali zuri sana. Ninaamini kuwa mimi ni mmoja wa makocha 20 bora,'' alisema Luis Enrique.
''Sababu kuna makocha 20 kwenye Primera Division.''
Akielezea umuhimu wa tuzo hizo ambazo hakuwepo wakati wa utoaji, enrique alisema lengo linahitajika kuwa mahali pengine.
''Sikuwa na mualiko, lakini bado ,unafahamu kwamba kawaida siwezi kuhudhuria hafla kama hizi.
''Na kwa wachezaji ambao hawakuwepo itakuwa vizuri ukiwauliza wenyewe.
''Sizani kama ni ni jambo la muhimu sana. Lengo ni kuinua soka la Hispania na wakurugenzi wanapaswa kuzingatia hilo.''

No comments:
Post a Comment