Saturday, October 22, 2016

KIPA WA TIMU YA VIJANA YA BROOKWOOD AONGEA KIHISPANIA BAADA KUZINDUKA ICU.

Reuben baada ya kupata nafuu.

Mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Reuben Nsemoh miaka 16 katika shule ya Geogia High School alipigania maisha yake baada ya majeraha ya kichwa aliyopata katika harakati za kuokoa mpira golini kwake akiwa yeye kama golikipa, na alipokuwa chumba cha watu mahututi alizinduka na kuanza kuzungumza lugha ya Kihispania kwa ufasaha, lugha ambayo hakuwai kuizungumza hapo awali jambo lililowashangaza watu wengi.
Reuben ambaye alijigonga kichwani baada ya kuukosa mpira hali iliyompelekea kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitalini na kuwa katika ICU kwa siku tatu, lakini jambo lililowashangaza zaidi ni hali ya kuamka na kuzungumza Kihispani kwa ufasaha bila kuzungumza lugha ya kiingereza anayoijua. 

Kinda huyoaliiambia WBS Radio Georgia kwamba huenda lugha hiyo amejifunza kutoka kwa marafiki zake na kaka zake ila anataka uwezo wake wa kuongea kiingereza hurudi.

Nsemoh alisema kwamba anataka kurudi tena uwanjani akaendelee na majukumu yake ya awali ya kipa, ingawa kocha wake amesema kwa sasa ni mapema mno kusema kwamba kinda huyo ataendelea kwenye timu hiyo.

No comments:

Post a Comment