Mtandao wa MARCA.COM uliweza kuuliza swali kwa watumiaji na mashabiki wa mtandao huo hapo jana baada ya majina ya wachezaji wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia ifahamikayo kama Ballon d'OR kutolewa na zali lilimdondokea nyota matata wa Barcelona Lionel Messi ambaye zaidi ya asilimia 58 ya mashabiki na watumiaji hao waliweza kumpigia kura yeye toka swali hilo liuzwe na mtandao huo.
Zaidi ya kura 100'000 ziliweza kusajiliwa ndani ya siku moja toka swali hilo ambalo liliuliza ''nani anaeweza kushinda Ballon d'OR?
Huku nyota Mreno Critiano Ronaldo alishinda Champion League na Euro 2016 akipata asilimia 26.6 ambaye kwa ameanza vibaya msimu huu, mbele ya Antonie Griezman wa Atletico Madrid aliyepata asilimia 3.24.

No comments:
Post a Comment