Thursday, October 13, 2016

MICKELSON AUNGA MKONO MAAMUZI YA TIGER WOODS.

Tiger Woods na Phil Mickelson.

Phil Mickelson ameunga mkono uamuzi uliofanywa na Tiger Woods wa kujiondoa kwenye michuano ya Safeway Open kama hakuwa tayali kimchezo.
Mickelson ambaye alitumia wiki moja akiwa na Woods kwenye Ryder Cup, anaelewa maamuzi yaliyofanywa na bingwa huyo wa mara 14. 

''Watu wote wa habari walikuja hapa, wakati alipoonyesha nia yake ya kurudi na yote hayo ilikuwa ni kuchambua uwezo wake kimchezo na vitu hivyo vikaongeza shinikizo,'' Mickelson aliiambia tovuti ya GolfChannel.com. 

''Kama hajisikii ni sawa, anahitaji kupumzika na kusubili. Wote tunamuunga mkono,''  

Mickelson anaamini kujiondoa kwa Woods kimewaumiza waandaji wa mashindano hayo.   

Pia akiamini kuwa Woods ni mchezaji mwenye mahesabu amabye atarudi mpaka pale atakapokuwa yuko sawa.   

''Wote tunataka Woods arejee tena, lakini tunahitaji aweze kurudi wakati yuko tayali kufanya hivyo, hivyo anapaswa kusubili.   

Mickelson ameeleza yote hayo baada ya Tiger Woods Jumatatu hii kwamba bado ana mipango juu ya mashindano ya Hero World Challenge Desemba mwaka huu.

 
 

 

No comments:

Post a Comment