Tuesday, October 18, 2016

SAHIN-MOURINHO ANASHINDA MCHEZO KWA MAZUNGUMZO YAKE YA MUDA WA MAPUMZIKO.

Nuri Sahin.
Kufuatia sare ya bila kufungana kati ya Liverpool na Manchester United hapo jana kiungo wa Borrusia Dortmund Nuri Sahin anaamini kocha waManchester United Jose Mourinho huwa anashinda mchezo kwa mazungumzo yake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza..
Kocha huyo wa Man United anafanya kila awezalo kuweza kushinda kwa kiwango kikubwa na hufanya kila awezalo kuweza kufanikisha hilo kwa mujibu wa Nuri Sahin.  

Sahin ambaye aliwahi kuwa chini ya kocha huyo akiwa Real Madrid ameelezea aina ya ufundishaji wa kocha huyo, Sahin alisema kwamba ''anashindaga mchezo kipindi cha mapumziko,'' aliiambia German Publication Socrates. 

''Maelezo yake ni ya ajabu, bado ninayo masikioni mwangu.  

''Kiukweli kila mchezaji anataka kushinda, lakini Mourinho anaunganisha ushindi. Anafanya kila awezalo, anapenda 
mafanikio.'' 

Sahin pia alimzungumzia kocha wa zamani wa Dortmund ambaye sasa ni kocha wa Liverpool Juregn Klopp, alisema ''kiukweli mbinu ni muhimu, mafunzo ni muhimu pia, lakini ubinadamu umekosa kitu kwenye hii biashara , kwa hiyo napenda watu kama Mourinho na Klopp.'' 

 


No comments:

Post a Comment