Tuesday, October 4, 2016

RONALDO BADO YUPO YUPO SANA

 Nyota wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo amewaeleza waandishi wa habari kuwa hana nia ya kustaafu soka kwa siku za karibuni kwani ana mipango ya miaka 10 kuwa katika soka.
Ronado ambaye alitokea Primer League akiwa na timu ya Manchester United na kujiunga na Real Madrid ya Spain, na kuongoza ufungaji kwenye Champions League.

Baada ya kufunga mabao 118 kwenye mechi zake 291 kwa Manchester United, Mreno huyo mpaka sasa ameshafunga mabao 352 kwa Madrid. 

Kazi yake imempa mataji manne ya Premier League, na moja la LaLiga na matatu ya Champions League na mwaka huu alishinda European Championship na timu yake ya taifa ya Ureno. 

Na kiungo huyo ameonyesha hasira yake kwenye soka baada ya kuonyesha kwamba hana nia ya kustaafu bali ana miaka kumi zaidi kwenye soka. 

''Maisha siyo kuhusu mpira,'' alisema nyota huyo mwenye umri wa  miaka 31 alipokuwa akifungua hoteli yake jijini Lisbon.  


''Ingawa soka ni shauku yangu kubwa, napaswa kufikiria juu ya siku zijazo.  

''Sina miaka mingi iliyobakia, ni kuhusu miaka 10 zaidi au chini ya hiyo, kwa hiyo napaswa kuangalia kwa siku zijazo.'' 


No comments:

Post a Comment