Wednesday, October 19, 2016

MASHABIKI COASTAL UNION TUNATAKA MPIRA NGUMI ZA NINI?

Kikosi cha Coastal Union ya Tanga.

Kitendo kilichofanywa na mashabikiwa timu ya Coastal Union ya jijini Tanga si chakiungwana kwa kumpiga mwamuzi Thoma Mkombozi kwenye Ligi Draja la Kwanza  msimu huu siku ya Jumapili.


Hali hiyo imepelekea Chama cha Waamuzi Taifa kupitia Mwenyekiti wake Siad Nassor kukaza waamuzi kuichezesha timu hio mpaka pale watakapotangaza. Kwenye mechio hiyo ya Jumapili timu hizo hadi zinaenda mapumziko KMC FC ilikuwa inaongoza moja bila lililofungwa na Augustino Ngata dakika ya pili ya mchezo baada ya kutumia makosa ya kipa wa Coastal Union Mansoor Mansoor huku mwamuzi akionekana kulimudu pambano hilo. Na kipindi cha pili wenyeji Coastal Union waliweza kusawazisha bao dakika ya 52 lililofungwa na beki Bakari Nendo  na la kuongoza lililofungwa na Seif Mkenza dakika ya 73. Lakini hali ya hewa ilitibuka pale mwamuzi huyo kutoa penati kwa KMC FC ndani ya dakika ya 83  iliyofungwa na Augustino Ngata  kitendo kilichoibua hasira kwa mashabiki hao kabla ya Rashi Roshwa kuongeza bao la tatu dakika ya 89 na la ushindi kwa wageni hadi mwisho wa mchezo.

Na ndipi mashabiki hao wakamvamia mwamuzi huyo na kuanza kumpa kipigo kabla ya kuokolewa na polisi na kumpa ulinzi.

Kiuhalisia mpira ni urafiki, mpira ni amani, na  burudani na sio kutumia mpira kuvuruga amani na siku zote kwenye mpira kuna kushinda, kufungwa na kutoa droo na kukubaliana na matokeo ya mchezo husika ndio kunaleta amani uwanjani. kitendo kilichofanywa na mashabiki wa Coastal union sio cha kiungwana kwa sababu kinawaharibia sifa nzuri ya klabu. Natumai marekebisho zaidi juu ya waamuzi wetu ambao mara nyingi wamekuwa wakionekana kumudu michezo yao husika wawapo uwanjani. Alamsiki.


No comments:

Post a Comment