![]() |
| Hans Pluijm. |
Sasa hivi kuna msemo ulioenea kwamba Mungu anakuona, na msemo huo naweza kuutumia kwenye hili sakata linaloendelea katika klabu ya Yanga kwa kocha wao Mholanzi Hans van Pluijm ambaye amejihudhuru kutokana na uongozi wa klabu hiyo kumleta kocha mwingine raia wa Zambia, George Lwandamina.
Yanga ambayo chini ya Pluijm iliogopeka na kuweza kuwapoteza kwa umbali mrefu watani wao wa jadi Simba SC, kwani Mholanzi huyo aliweza kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululuizo na kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shiirikisho la Afrika. Pluijm mpaka anajiuzulu tayali alikuwa na mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo na mkataba huo alisaini mwanzoni mwa msimu huu. Kwa kinachoendelea sasa ndani ya klabu kongwe nchini ya Yanga Africans ni dhahiri mtani wake Simba SC anafaidika nacho kwa kuhimarisha kasi ya ushindi kwa msimu huu.
Kocha huyo Mzambia ambaye inadaiwa kuletwa na Kampuni ya Yanga ya Yetu inasemekana bado ana mkataba na Zesco ya Zambia anadaiwa kuja kufanya mazungumzo na mwisho na yanga kabla ya kurudi Zambia na mazungumzo hayo ndiyo yataamua kama atakuwa mrithi wa Pluijm au lah.
Kwa zaidi ya mwezi sasa kumekuwa na tetesi za Yanga kubadili benchi
la ufundi kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu kwa sasa. Kwa mtazamo wangu Pluijm alikuwa kocha sahihi kwa Yanga kwani aliweza kuendana na presha ya wachezaji ndani ya klabu hiyo.
Yanga iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 21 nyuma ya Simba inayoongoza kwa pointi 29.

No comments:
Post a Comment