Monday, October 24, 2016

NINA FURAHA ZAIDI NIKITOKEA BENCHI NA KUFUNGA-MORATA.

Alvaro Morata dakika chache akitokea benchi aliweza kudhihirisha umuhimu wake wenye timu yake ya Real Madrid baada ya kuifungia bao muhimu kwenye mchezo dhidi yao na Athletic Bilbao, na ameelezea furaha yake juu ya jambo hilo.
Mchezaji huyo mwenye miaka 24 ambaye mara kwa mara anaanzia benchi jambo ambalo linaonyesha halimsumbui kwani amekuwa msaada wa timu yake kila inapokuwa na hali mbaya Morata alisema ''pale ninapotokea benchi na kufunga bao, kwangu ni sawa kwasababu ninachofanya ni kuisadia timu kufanya vizuri.''
''Itakuwa upuuzi kuweka mbele matatizo yangu ya kibinafsi mbele ya timu.''

''Siku zote ninataka kucheza hapa na ninakubaliana na maamuzi ya kocha.''
Morata ambaye aliielezea mechi hiyo ambayo ilikuwa ngumu kwa Real Madrid ambapo ilifananishwa na ''El Clasico'' alisema,
''Ilikuwa mechi ngumu, na wanatimu nzuri ambayo ni ngumu kuifunga, na hatukuwa kwenye ubora wetu.
Kwenye mchezo huo ambao Madrid walianza kuongoza kwa bao la Isco kabla ya Athletic kusawazisha kupitia mchezaji wao Keylor Navas na kufanya matokeo 1-1.

No comments:

Post a Comment