![]() |
| Ozil akifunga moja ya mabao yake hapo jana dhidi ya Ludogorets. |
Baada ya hapo jana timu yake kuibuka na ushindi wa mababo 6-0 dhidi ya Ludogorets, kocha wa Arsenal Arsene wenger amemsifia nyota wake Meut Ozil kuwa ana ladha ya mabao baada ya hat-trick aliyoifunga kwenye mchezo huo.
Mshambuliaji huyo wa Arsenal alifunga mabao matatu kwenye ushindi huo kwenye mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Emirates.
Wenger alisema ''inaonekana amepata ladha ya kufunga mabao sababu alikuwa anaenda nyuma zaidi ,'' aliongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari.
''Hapo kabla, alikuwa anapenda kuwa na mpira na kutoa pasi.
''Tunahitaji awe mtoaji pasi na mfungaji na ikaonekana kama yuko taratibu sana kuwa kwenye nafasi bora.''
![]() | |
| Wachezaji wa Arsenal wakishangilia ushindi kwenye chumba cha kubadilishia nguo. |
Kwenye mchezo huo mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Alexis Sanchez na Theo Walcott. Na matokeo mengine ya michezo mingine ni kama ifuatavyo-
Bayern Munich 4-1 PSV Eindhoven
Paris Saint-Germain 3-0 Basel
Dynamo Kiev 0-2 Benfica
Napoli 2-3 Besiktas
FC Rostov 0-1 Atlético Madrid


No comments:
Post a Comment