![]() |
Hans Pluijm na Mh Mwigulu Nchemba. |
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ameweza kumrejesha kundini kocha wa Yanga,Hans-van-der-Pluijm kuendelea na kibarua chake cha kuinoa Yanga ambako tayari
alishafungashiwa virago.
Pluijm alijiuzulu mapema wiki hii baada ya kukerwa na uongozi wa
klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina bila kumtaarifu,
akisema huko ni kumvunjia heshima. Kocha huyo akakataa hadi nafasi ya
Ukurugenzi wa Ufundi ambayo inasemekana Yanga ilitaka kumpa baada ya
kumleta Lwandamina kuwa kocha mkuu.
Mh Mwigulu alifanikiwa na jitihada zake za kumrudusha kocha huyo ambapo aliendesha vikao na viongozi wa
Yanga na kocha huyo kwa siku tatu mfululizo na hatimaye jana kocha huyo
akakubali kuendelea na kazi yake ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.
Akizungumza na HabariLeo, Nchemba alisema hajaona sababu ya msingi ya
Pluijm kuondoka kwa kuwa kocha huyo ameongoza Yanga kwa mafanikio
makubwa na kwamba mechi zilizosalia kwenye ligi ni ngumu kwa upande wao.
“Mimi ni mwanachama hai wa Yanga, Hans kuna masuala alitofautiana na
uongozi ya kiutawala, ambapo uongozi ulikuwa ukimshinikiza mwalimu,
akapata hasira ndio akaandika barua ya kujiuzulu. “Lakini nimezungumza
na pande zote mbili na nimeyaweka sawa, kama uongozi una mipango mingine
ifuate taratibu za kumuondoa kwa kuwa kocha bado ana mkataba wa mwaka
mzima na Yanga, na suala la malipo klabu itaendelea kumlipa kama
kawaida,” alisema Nchemba
Mholanzi huyo ambaye mpaka anaondoka Yanga tayali alishaiongoza Yanga katika jumla ya mechi 124, za Ligi na kimataifa
akishinda 77, sare 25 na kufungwa 22.
Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na
kufungwa mbili, wakati katika mechi 106 za tangu mwaka jana, alishinda
66, sare 19 na kufungwa 20.
Wakati Nchemba akisema hayo, Katibu Mkuu wa
Yanga, Baraka Deusdetit alisema klabu hiyo imekataa ombi la kujiuzulu
kwa Pluijm kwa kuwa haioni sababu ya kuachana na Mholanzi huyo.
Lakini baada ya kuwaaga wachezaji siku moja kabla ya mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu timu ikishinda 4-0,
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba aliingilia kati suala hilo. Na tayali uongozi wa Yanga umemuandika Pluijm barua ya
kumuomba radhi na kumuangukia arudi kazini akitakiwa kuongoza benchi la
ufundi la Yanga dhidi ya Mbao Fc kesho.
No comments:
Post a Comment