![]() |
| Lukas Modric. |
Klabu ya Real Madrid imethibitisha kiungo wake Lukas Modric ameongeza mkatba utakao muweka Santiago Bernabeu mpaka 2020. Madrid walimpa mkataba mpya Jumatano iliyopita Toni Kroos utakaomuweka klabuni hapo mpaka 2022, ni kama Los Blancos hawataki kupoteza muda juu ya viungo kwa ajili ya mustakabli wa baadaye wa klabu hiyo.
Taarifa ya klabu hiyo ilisema ''Real Madrid na Lukas Modric wamefikia makubaliano ya kuongeza mkataba utakaomuweka mpaka June,30 ,2020.''
Modric ataonekana Jumatano kabla ya 1.30 mchana kujadili juu ya mkataba huo mpya , mchazaji huyo wa zamani wa Tottenham ambaye amekuwa muhimili mkubwa kwa Zinedine Zidane ndani ya klabu hiyo.

No comments:
Post a Comment