![]() |
| Pep Guardiola. |
Baba mzazi wa kocha wa Manchester City Pep Guardiola, Valenti Guardiola ameweka wazi kwamba mwanae huyo hatoweza kurudi kuifundisha Barcelona au timu ya taifa ya Hispania.
Guardiola ambaye aliwahi kuwa mchezaji na kocha wa Barcelona kwa mafanikio makubwa kwa timu hiyo kwa uwanjani na kwenye benchi la ukocha kabla ya kutimkia Bayern Munich ya Ujerumani na sasa yupo Manchester City ya Uingereza.
Hata hivyo, Valenti hafikiri kuwa siku moja mwanae huyo atakuwa na mawazo ya kurudi Hispania kwenye timu aliyokuwepo hapo awali.
''Pep kurudi Barcelona? kufanya nini, kijana wa kuokota mipira? Guardiola Sir aliiambia Cadena Ser.
''Simuoni nikimuona akirudi pale.
''Muda wake kwa klabu ulikuja na umeondoka sidhani kama kuna namna ya yeye kurudi kama kocha.
Valenti ambaye anaonekana kama kumpangia mwanae majukumu ya kumchagulia kazi ya ukocha hata kwenye taifa lake la Hispania. Baba huyo alisema ''sidhani kama Pep anaweza kuchagua kuifundisha timu ya taifa.''
''Lakini siwezi kumuona akichukua jukumu la timu ya taifa.''
''Sina chochote cha kupingana na mtu yoyote lakini hayo ni mawazo yangu.
''Mwisho wa siku, sijui hatafanya nini na mimi sio wa kusema afanye nini.''

No comments:
Post a Comment