![]() |
Frank Ribery. |
Winga wa Bayern Munich Mfaransa Franck Ribery amejitetea kutokana na malalamiko ya kuonekana kama mchezaji mtukutu na mkorofi na kusema kwamba anakuwa katika hali hiyo pale tu anapoona adui anataka kumjeruhi.
Winga huyo amegonga vichwa vya habari kwa sababu ya makosa zaidi ya mara moja msimu huu, akihusishwa kwenye matukio dhidi ya wachezaji Felipe Melo, Felix Passlack na Nicolai Muller.
Lakini Ribery amesisitiza kwamba yeye sio mchezaji mbaya akiwapo uwanjani.
''Ninafahamu kwamba nahitaji kuwa makini. Lakini ningependa kuweka wazi kwamba mimi sio mchezaji mkorofi,'' mchezaji huyo mwenye miaka 33 aliiambia Sport Bild.
''Kuna wakati napoteza upole wangu kwa muda, lakini pale tu ninapoona adui yangu anataka kunihumiza. Sina tatizo na uzito au ugomvi, lakini ninakuwa hivyo nikiona mtu anataka kunitoa nje ya mchezo.
''Lakini kamwe sina lengo la kumuumiza mtu yoyote. Kwani kila kitu nasahau dakika chache mbele.''
No comments:
Post a Comment