![]() |
Jose Mourinho na Arsene Wenger. |
Peter Cech ana amini kuwa kocha wa Arsenal, Arene Wenger na Jose Mourinho wa Manchester United wako sawa zaidi kimtazamo.
Makocha hao ambao wanapitia kipindi kigumu cha uhusiano toka Mreno huyo ajiunge na Chelsea mwaka 2004 huku wakitupiana maneno makali zaidi ya mara moja.
![]() |
Peter Cech akiwa Arsenal. |
Cech ambaye ameshakuwa chini ya makocha wote hao wawili, ameelezea jinsi makocha hao wanavyochukia kupoteza mchezo na ndio kitu kinachowapa mafanikio.
''Wenger na Mourinho wako tofauti lakini kuna kitu kimoja wanachofanana ni kwamba hawapendi kufungwa.'' golikipa huyo wa Arsenal aliwaambia waandishi wa habari.
''Na hilo nadhani ndilo linalowafanya waendelee kufanikiwa kwa wote wawili.
''Sababu huwezi kumudu kwa muda mrefu namna hiyo kama huna dhamira na hasira kama hutofanya lolote kujiepusha na kipigo.
No comments:
Post a Comment