![]() |
| Uwanja wa Rolo Borici ambao mchezo huo utapigwa. |
Leo Spain inashuka dimbani dhidi ya Albania kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Russia.
Huku Albania ikiwa kiongozi wa kundi G ambapo inaonekana kwamba sio timu rahisi ya kukutana nayo, hivyo kwa upande wa Lopetegui usitarajie njia rahisi ya kuelekea Russia kupitia kwa Albania kwani unatarajiwa kuwa mpambano mkali kati yao.
Baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Macedonia nyumbani na ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya Liechtenstein, vijana wa Gianni De Biasi wanaamini uwezo wao dhidi ya kuwakabili Spain na kuwapa nguvu kwenye mzunguko wao wa mechi.
Huku ikiwa mabeki ni uti wa mgongo kocha wa Spain atachagua kati ya mabeki wataokaosaidiana kwenye mechi ya leo ambao ni Nacho Monreal (Arsenal), Javi Martinez (Bayern Munich), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Sergi Roberto (Barcelona), Nacho (Real Madrid), and Dani Carvajal (Real Madrid).
Huku nafasi ya kiungo na mbele akitumia mfumo wa 4-3-3, hali itayomfanya Lopetegui kuwa na majaribio mengi. Huku washambuliaji wakiwa Nolito (Manchester City), Diego Costa (Chelsea), Lucas Vazquez (Real Madrid), Vitolo (Sevilla), Alvaro Morata (Real Madrid), and Jose Callejon (Napoli).
Na kwa nafasi ya viungo David Silva (Manchester City), Thiago Alcantara (Bayern Munich), Saul Niguez (Atletico Madrid), Koke (Atletico Madrid), Andres Iniesta (Barcelona), Sergio Busquets (Barcelona), and Isco (Real Madrid yeyote anaweza kuanza kwenye mchezo huo ambao unaonekana mgumu kwa timu zote mbili.

No comments:
Post a Comment