Kiungo wa Manchester united Paul Pogba ameweka wazi kwamba sare yao ya 0-0 dhidi ya Burnley ilimfanya ajisikie kupata uchizi, kwenye mchezo huo Man United walipata nafasi 37 za kushambulia goli la Burnley lakini walishindwa kuwafunga . Inakuwa mfulululizo wa sare kwa United kupata Old Trafold kwenye Premiere League.
Kiungo huyo wa Ufaransa baada ya mapumziko aliboresha mashambulizi kwa Msweden Ibramovic ili kuweza kumsaidia kumaliza ukame wa mabao lakini pia haikuwasaidia kuliona lango la Burnley.
Pogba ambaye alikuwa Wembley Jumapili hii ambapo kulikuwa na mchezo wa NFL kati ya Washngton Redskins na Cincinnati Bengals kama mgeni kwa Joshua Norman.
''Nilikuwa mwendawazimu pia kama yeye akimaanisha Redskins, lakini unajua kwamba huu ni mchezo.
''Kusema ukweli, nilijisikia kama nimepoteza baada ya kukosa kufunga bao, lakini hayo yote ni mchezo tu unajua. Wewe unachotakiwa kufikiria ni juu ya mchezo uajo na kufanya vizuri.
United imeshinda mechi moja kati ya saba za mwishoni kwenye Ligi. Na Mourinho atawaongoza kuelekea mchezo wao dhidi ya Fenerbace katika Europa Ligi katika mechi yao ya nne msimu huu kwa Ulaya kabla ya kuwavaa Swansea siku ya Jumapili ijayo.
No comments:
Post a Comment