Tuesday, October 25, 2016

SCOLARI AONGEZA MKATABA NA GUANGZHOU.


Mabingwa wa China timu ya Guangzhou Evergrande Taobao wamempa mkataba mpya wa mwaka mmoja kocha wao Luiz Felipe Scolari. Mkataba huo mpya ni pamoja na fursa ya mwaka wa pili baada ya Evergrande kuweka rekodi mpya ya kushinda kwa mara ya sita taji la Chinese Super League wiki iliyopita.

Scolari mwenye miaka 67 aliwahi kushinda taji la Kombe la Dunia 2002, alikuwa mbioni kuachana na klabu hiyo baada ya mkataba wake kufikia mwishoni  na kocha wa zamani Marcello Lippi alishafikia makubaliano na klabu hiyo, lakini Evergrande walivunja makubaliano hayo baada ya mkongwe huyo kuchukua jukumu la kuinoa timu ya taifa ya China Jumamosi iliyopita.

''Bila shaka tunaamini kwamba Scolari, ni mmoja wa makocha bora duniani ataisadia Guangzgou kuendelea kuimarisha nafasi yao ya uongozi.''  Taarifa ya klabu hiyo ilisomeka hivyo kwenye mtandao wao.

Scolari ambaye amepata mafanikio kwenye klabu hiyo toka ajiunge nao mwaka 2015 baada ya kumrithi Fabio Cannavaro.Mbrazil huyo ameiongoza Evergrande kwenye michuani ya CSL na AFC Champions League na kuweza kupata mafanikio ndani ya msimu, kabla ya kurudi kwenye Lligi msimu huu.

Kocha huyo mkongwe anaweza kuongeza taji lingine na Evergrande ambao watacheza na Jiangsu Suning kwenye China FA Cup.


No comments:

Post a Comment