Arsenal ni timu ambayo inafanya vizuri mwanzoni mwa msimu kiasi cha kuweza kuwaaminisha mashabiki wake kwamba wanaweza kushinda taji kwa msimu huo lakini hali inakuwa tofauti kabisa baadaye wanapoanza kuboronga lakini safari hii kocha wa Arsenal Arsene Wenger
amesema kuwa wana fursa nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu kwa
mara ya kwanza tangu washinde taji hilo mwaka 2004.
![]() |
| Arsene Wenger 2004 aliposhinda taji hilo. |
Wenger akizungumza
katika mkutano wa kila mwaka wa klabu hiyo,Wenger mwenye umri wa miaka
67,alisema kuwa mshindi wa taji la ligi kuu atakuwa na kati ya pointi 82
na 86 mwaka huu.
Alisema: Hii leo tuko katika nafasi nzuri zaidi
ya kuwania taji la ligi ya Uingereza ikilinganishwa na miaka mitano au
sita iliopita.
Ninaamini tuna timu nzuri katika ligi yenye ushindani mkubwa.
Arsenal
ni wa pili katika jedwali la ligi,ikiwa ni mojwapo ya timu tatu zenye
pointi 20 na wako katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao.
Wenger anasema kuwa anafikiri kwamba anahitaji pointi 62 kutoka kwa mechi 29 zilizosalia kushinda taji .
Leicester ndio mabingwa wa taji hilo msimu uliopita.
''Baada ya mechi 9 ,tuna pointi 20,ikimaanisha kwamba ubingwa huo utaamuliwa na kati ya pointi 82 na 86'',alisema.


No comments:
Post a Comment