Tuesday, October 11, 2016

SITOWEZA KUICHEZEA BARCELONA -CASEMIRO.

Image result for casemiro injury images against espanyol
Casemiro.
                           

Nyota wa Real Madrid Casemiro amesisitiza kwamba hatoweza kuja kujiunga na  timu ya wapinzani wao Barcelona.
 Kiungo huyo wa Brazil alikuwa na wakati mgumu Santiago Bernabeu chini ya kocha aliopita Rafael Benitez, lakini sasa ni tegemeo kwenye mipango ya kocha Zinedine Zidane ndani ya Madrid. 

Kuumia kwake mguu na kukaa nj'e kwenye mchezo wao walioshinda 2-0 dhidi ya Espanyol Septemba 18 umedhihirisha umuhimu wa mchezaji huyo baada ya Madrid kuwa na maendeleo yasiyoridhisha kwa kupata sare nne kwenye michezo yao. 
Image result for casemiro injury images against espanyol
Casemiro akitolewa nj'e kwenye mchezo wa Madrid dhidi ya Espanyol.
''Sitoweza kuichezea Barcelona, kwa sababu kwa Hispania mimi ni shabiki wa Real Madrid,'' alisema. 

''Real Madrid ni zaidi ya nilivyotarajia, napenda ninavyoamka asubuhi na kwenda  Valdebebas (kambi ya mazoezi ya Real Madrid). 

''Napenda ninavyokuwa na wachezaji, tukitaniana, kufanya kazi na kujifunza. Najaribu kuishi maisha ya soka kila siku.

''Real Madrid ni maisha yangu leo.'' 


 

No comments:

Post a Comment