Tuesday, October 11, 2016

VIDEO YA RASHED AL-HAJJAWI YA YOUTUBE YAMPA MAISHA JUVENTUS.

Klabu ya Juventus ya Italia inataka kumsajili Rashed Al Hajjawi kwenye timu ya watoto chini ya umri wa miaka kumi kufuatia kuona video ya mtoto huyo kwenye mtandao wa youtube.
Mpalestina huyo aliyezaliwa nchini Norway mwenye vipande vingi vya video youtube vinavyomuonesha akionyesha uwezo wake wa kumiliki vizuri mpira, ameamua kujiunga na akademi ya miamba hiyo ya Serie A ya Italia baada ya kuutembelea uwanja Juventus. 

Huku klabu hiyo ikitangaza kumsajili wikiendi hii.

Kutokana na kuongezeka na kuendelea kwa vyombo vya kijamii na upatikanaji mpana wa teknolojia, idadi ya kuwapata watoto wenye vipaji itazidi kugundulika kila siku.

Rashed hana tofauti na mtoto Karamoko Dembele kutoka Celtic kucheza kwenye timu ya U-20 akiwa na miaka 13. 

Kwa Rashed ambaye ndio kwanza ana umri wa miaka 10 na ameshaonyesha uwezo mzuri kwenye soka, ana njia ndefu ya kwenda kuelekea kutimiza ndoto na malengo yake ya baadaye.

No comments:

Post a Comment