Leo kulikuwa na mchezo wa Premier League maarufu ''London Derby'' kati ya mahasimu wa jiji moja la London kati ya Arsenal na Tottenham Hotspurs ambapo mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates ambapo mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Kwenye mchezo huo ambao The Gunners walipata bao hilo baada ya Kevin Wimmer kujifunga katika harakati za kuokoa mpira kabla ya Spurs kupata penati baada ya Mousa Dembele kuchezewa rafu eneo la hatari iliyowekwa wavuni na mchezaji wao aliyekuwa nje kwa majeruhi Harry Kane dakia ya 51 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.Matokeo hayo yanafanya kuipunguza kasi Arsenal kwenye mbio zake za taji la Ligi hiyo ambapo hawakupoteza mchezo hata mmoja toka msimu huu uanze.
No comments:
Post a Comment