Sunday, November 6, 2016

MIAKA 30 YA FERGUSON MANCHESTER UNITED


Sir Alex Ferguson akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari 1986.
Sir Alex Ferguson ni kocha raia wa Scotland ambaye aliweza kuifundisha klabu ya Manchester United kwa mafanikio makubwa kiasi kuwa timu iliyokuwa ikiogopeka kwa kipindi chake. Ferguson alikabidhiwa timu hiyo mnamo Novemba 7 1986 mpaka 2013 ambapo aliamua kustaafu kuwa kocha. Kwa kipindi chake cha miaka 26 alichokuwa Man United aliweza kushinda mataji 38 huku 13 yakiwa ya Premier League, 5 ya FA Cup na 2 ya Uefa Champions League akiwa meneja aliyekaa muda mrefu Manchester United.
Na kwa kipindi chake aliweza kuwa na usajili uliokuwa bora na usajili uliokuwa mbovu katika historia ya Manchester United.

Wachezaji watano ambao walikuwa bora katika usajili wa Ferguson.
1.Peter Schmeichel ni golikipa ambaye mpaka sasa anakumbukwa na wapenzi, mashabiki na wadau wa Manchester United kwa uwezo wake aliokuwa nao golini.
2.Cristiano Ronaldo huyu alimnunua kwa ada ya Paundi milion 12 na alimuuza kwenda Real Madrid kwa ada ya paundi milion 80 na hakika ilikuwa biashara iliyofanyika kihalali kwani Ronaldo alikuwa kwenye kiwangi bora zaid kwa wakati huo.
3.Rud Van Nistelrooy Paundi milion 19 iliyoweza kuweka mafanikio klabuni hapo kwani alikuwa mashine katika ufungaji kwenye mechi zake.
4. Eric Cantona huyu hakuna asiyemfahamu katika historia ya Manchester united kwa kipindi alichokuwepo klabuni hapo, Fergie alimnunua kwa ada ya Pauni milion 1.2 mwaka 1992 ni kama vile alinunua magoli na uwezo uliokuwa mkubwa.
5.Roy Keane alisajiliwa kwa rekodi ya paund milion 3.75 akitokea Nottigham forest 1993, Keane ambaye alionekana kama wa bei ndogo aliitumikia klabu hiyo kwa miaka 12 lakini aliitumikia klabu hiyo kwa jasho na damu kiasi mpaka leo mchango wake kwa timu hiyo unakumbukwa.

N a wachezaji ambao walikuwa usajili mbovu kwa Fergie.
1.Massimo Taibi huyu alikuwa kipa ambaye Fergie alizani kanunua mrithi wa Schmeichel lakini haikuwa hivyo kwani alicheza mechi nne na kutolewa kwa mkopo January ambapo united walipata hasara ya paundi milion 2 toka kwake kwani alisajiliwa kwa paundi milion 4 mwaka 2001.
 
Massimo Taibi.

2.Juan Sebastian Veron ulikuwa usajili uliovutia kila mtu lakini veron alishindwa kuonyesha thamani yake kwa red devils alisajiliwa kwa paundi milion 28 mwaka 2001.
 
Fergie na Veron 2001.

3.Diego Forlan Fergie aliweza kumuacha Boro kwa ajili ya Forlan ambaye walimuahidi mshahara mzuri lakini Forlan alicheza kiwango kibovu akiwa na jezi ya Man United.
4.Bebe alisajiliwa mwaka 2010 kwa ada ya paundi milion 7.4 lakini hakuweza kuonyesha kiwango chochote hali iliyomfanya akose timu za kutaka kumsajili.
5.Djemba Djemba  alisajiliwa kwa paundi milion 3.5 milion mwaka 2003 akitumainiwa kumrithi Roy Keane lakini alishindwa kuweza pengo la Roy Keane na kuishia mchezaji wa hasara kwa United.

No comments:

Post a Comment