Monday, November 7, 2016

ATLETICO INAPASWA KUJIWEKA SAWA ILI KUSHINDA DERBY-GABI.

Image result for gabi images with atletico



Kuelekea mchezo wao na mahasimu wao wa jiji moja Real Madrid kiungo wa klabu ya Atletico Madrid Gabi amewatahadharisha wachezaji wenzake kuelekea mchezo wao baina ya mahasimu wao hao baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, ya kwamba wanapaswa kujihimarisha ili waweze kushinda mchezo huo.
Vijana hao wanaotokea kwenye Uwanja wa Vicente Calderon wameshapoteza michezo miwili kati ya mitatu kwenye LaLiga na wameshuka mpaka nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi hiyo, wakiwa nyuma ya pointi sita kwa Real Madrid anayeongoza kwenye msimamo.

Gabi ameonyesha umuhimu wa kuongeza kasi dhidi ya vijana wa Zinedine Zidane na kuimarisha uhimili na udhibiti ambao ni umeonekana kuwa muhimu na mafanikio chini ya Diego Simieno.

''Utakuwa ni mchezo muhimu kwetu. Ni muhimu sababu hatutakuwa tayali kuwaachia real Madrid kwenda mbali zaidi ya uongozi kwetu,'' Gabi aliwaambia AS.

''Tunahitaji kuwa shingo kwa shingo na wao, lakini tunahitaji kujihimarisha kama tunataka kushinda ''derby''.

''Tunahitaji kurudi na kuwa timu ambayo ina uhimiri kwa nyuma na tunapaswa kufanya kazi yetu ya kuimarisha timu.

No comments:

Post a Comment