Tuesday, November 8, 2016

NADAL KUREJEA DIMBANI DECEMBER MWAKA HUU.

                               Image result for rafael nadal images in abu dhabi


Bingwa mara 14 wa grand Slam Rafael Nadal amethibitisha kurejea dimbani kwenye mihuano ya Mubadala World Championshipjijini Abu Dhabi mwezi ujao. Nadal ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya kiuno kwa mwaka huu, hali iliyomrazimu kujiondoa kwenye michuano ya French Open na kukosa Wimbledon.
Nadal ambaye alirudi kwenye Rio Olympics mwezi Agosti na kushinda medali ya dhahabu sambamba na Marc Lopez kwenye mchezo wa wachezaji wawili, lakini alipata shaba kwenye mchezo wa mtu mmoja mmoja dhidi ya Kei Nishikori.

Hata hivyo, bingwa huyo namba moja wa zamani tatizo la kiuno liliendelea kumsumbua na kufanya kuwa na msimu mbaaya kwa mwaka huu 2016. Na hivyo anatarajia kurudi ulingoni ili kutetea taji lake kwenye Umoja wa nchi za Kiarabu ''UAE''.

Nadal alithibitisha taarifa hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitte.

''Ninafuraha kuwajulisha kuwa mashindano yangu ya kwanza yatakwa Abu Dhabi kwenye Mubadala World Tennis Championship mwezi Desemba,'' aliandika Muhispania huyo. 


No comments:

Post a Comment