Monday, November 7, 2016

MESSI AFIKISHA MABAO 500 BARCELONA.


Bao lake dhidi ya Sevilla Jumapili ya jana limeweza kufikisha idadi ya mabao 500 kwenye klabu yake ya Barcelona. Muargentina huyo alifunga bao hilo ndani ya dakika ya 43 wakitoka nyuma na kushinda 2-1 kwenye Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan.
 Linakuwa bao la 16 kwa msimu na bao la 27 kuifunga Sevilla katika maisha yake ya soka, na kufanya kutimiza idadi ya mabao 500, Messi mwenye miaka 27 anatimiza idadi hiyo kutoka kwenye mechi 592 za klabu hiyo ya Hispania.

Barcelona ambayo walivunja rekodi baada ya mechi, kwa mabao 320 ya Messi kwenye LaLiga ikiwa ni mchango mkubwa kwenye idadi yake. Barcelona ambayo rekodi yake ni mabao 469 kwa klabu kwa jina lake na idadi hiyo inajumuisha pamoja na mechi za kirafiki.




No comments:

Post a Comment