Wednesday, November 9, 2016

CECH AIPA UBINGWA WA PREMIER LEAGUE ARSENAL.


Golikipa wa Arsenal Peter Cech anaamini timu yake itaweza kufanya vizuri kwenye mbio za kuwania taji la Premier League na kushinda taji hilo kwa msimu huu. Arsenal ambao wako nafasi ya nne kimsimamo wakiruhusu kufungwa mara moja tu kwa msimu huu.
 
Cech ambaye alishinda taji hilo akiwa Chelsea, anaamini kwamba Arsenal iko kwenye nafasi ya kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka 2004.

''Nafikiri ubora tulionao ni nguvu kubwa kwenye msingi,'' Cech aliongea kwenye mtandao wa klabu yake.

''Pae tulipokosa bahati kwa kipindi kirefu cha kuwa na majeruhi kwa msimu uliopita, ilitubidi kutumia wachezaji walewale kwenye michezo mingi na kupoteza nguvu kwenye kipindi chote cha msimu.

''Tulipoteza pointi kwa sababu tilishindwa kuzunguka. Kwa msimu huu tuna msingi mkubwa, unaaweza kuona kwenye Ligi ya Mabingwa na makombe ya ndani na Premier league tunatumia wachezaji tofauti au wachezaji walewale.

''Meneja ana machaguo yake na nafikiri tunafaidika nayo kwa mbali. Kila mtu anajiweka sawa kwenda kwenye mchezo.''

Arsenal walifanikiwa kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya Leicester City ikiwa ni mara ya kwanza toka 2004-2005.

No comments:

Post a Comment