Beki wa timu ya Brazil Dani Alves amesisitiza kwamba timu yake haimuogopi Lionel Messi pale watakapokutana na argentina kwenye mechi ya kuwania kufuzu kombe la Dunia. Mahasimu hao watakutana Alhamisi hii Belo Horizonte kwenye nafasi ya CONMEBOL.
Brazili ambao wako nafasi ya kwanza baada ya kupoteza mechi moja kati ya kumi kwenye kufuzu, huku Argentina ikiwa nafasi ya sita.
Alves ambaye kwa sasa yuko Juventus lakini alikuwa timu moja na Messi alipokuwa Barcelona, beki huyo wa Juventus amesema kwamba Brazil wanapaswa kuacha uwoga wa kumuogopa nyota huyo.
''Uwoga hauitajiki kwenye soka. Bali kuna heshima kubwa,'' aliwaambia News Conference Jumanne hii.
''Ni sawa kwamba kuna heshima ya ujumla kwa Messi na kwa timu yake ya taifa ya Argentina.
''Ni kama kuamini kwamba kuna heshima kwa wacheazji wetu na kwa timu yetu ya taifa kwa ujumla.
''Kwa hiyo tunaelekea kwenye mchezo mzuri na kuendeleza ukuaji na ubora wetu bila kujali nani aliyekuwepo ndani ya timu.
No comments:
Post a Comment