Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara unafikia tamati leo na kesho. Simba leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya kucheza Prisons huku Yanga kesho akicheza na Ruvu Shooting.
Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya
kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa
wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, mwaka huu
Wafungaji wanaoongoza kwenye raundi ya kwanza.
Kwa upande wa wafungaji bora mpaka sasa Shiza Kichuya wa Simba
anazidi kuwakimbiza ikiwa na mabao tisa hadi sasa, akifuatiwa kwa karibu
na Amis Tambwe wa Yanga mwenye mabao saba akikabana koo na Rashid
Mandawa wa Mtibwa Sugar naye ana mabao saba.
Simon Msuva wa Yanga mabao sita huku wenye mabao matano wakifungasha
wachezaji sita ambao ni Omary Mponda, Riffat Khamis (Ndanda),
Abdulrahaman Musa (Ruvu Shooting), Obrey Chirwa, Donald Ngoma (Yanga) na
John Bocco (Azam).
No comments:
Post a Comment