Thursday, November 10, 2016

HARDEN AISAIDIA ROCKETS KUPETA MBELE YA SPURS NBA.


Hekaheka ya msimu mpya wa NBA umeendelea hapo jana na mchezaji James Harden alikuwa shujaa kwa timu yake ya Houston Rockets kwenye ushindi dhidi ya San Antonio Spurs kwenye ligi hiyo ya kikapu maarufu nchini Marekani, huku Golden State Warriors wakishinda pia.
Harden ameweka rekodi ya kufunga mara tatu-mbili kuiongoza Rockets kushinda 101-99 Jumatano ya jana. Matokeo hayo yanaifanya Spurs kupoteza mchezo wa tatu mfululizo kwa nyumbani.



Huku Warriors wakishinda kwa urahisi dhidi ya Dallas Mavericks, kwa pointi 116-95. Huku nyota wa timu hiyo Steven Curry akifanya vizuri.

No comments:

Post a Comment