![]() |
Cristiano Ronaldo 2003 alipokutana na Man U akiwa Sporting CP. |
Aliyekuwa kocha wa Sporting CP Fernando Santos anatamani kama angerudisha muda nyuma basi asingemchezesha Cristiano Ronldo kwenye mechi iliyowakutanisha na Manchester United, mechi ambayo imeweza kumpa maisha mazuri nyota huyo wa Kireno kwa sasa.
Mwaka 2003, Ronaldo aliingia kucheza dhidi ya Man United kwenye mchezo wa awali kabla ya msimu kuanza ndipo AlEX Ferguson alipomuona Mreno huyo na bila kupoteza muda wakamsajili kwa haraka akiwa na miaka 18 tu.
Usajili uliobadirisha maisha yake ambapo alishinda na United mataji matatu ya Premier League na Klabu Bingwa kabla ya kuhamia kwa vigogo wa Hispania Real Madrid , ambapo ameshinda mataji makubwa kwa LaLiga toka 2009 na Kombe la Euro 2016.
Akionyesha majuto kwa kumchezesha na kumuuza mchezaji huyo bingwa mara tatu wa Ballon d'OR miaka kumi tatu iliyopita.
''Nilikuwa kocha kipindi ambacho Sporting CP wanancheza na United. Nilimchezesha Ronaldo na baadae nikatamani nisingemchezesha,'' santos alisema hayo jana JUmatano.
''Wiki ambayo Ricado Quaresma aliondoka na kujiunga na Barcelona, alafu siku mbili mbele Ronaldo akawa yuko njiani kuelekea Manchester United.
''Kurudisha nyuma siku hizo, sikuwahi kufikiria kuwa miaka 13 iliyopita wote wawili wataweza kushinda taji la Europe wakiwa na timu ya taifa.''
No comments:
Post a Comment