Soka linaweza kuwa baya kama kutakuwepo hamna watu waongeaji kama Mourinho kwa mujibu wa rais wa FiFa Giani Infantino. Mreno huyo ambaye kwa sasa anainoa klabu ya Manchester United mara nyingi amekuwa akiingia kwenye mikwaruzano na maoni chanya kwenye kazi yake na makocha wa timu pinzani au waamuzi.
''Mourinho ni mtu anayechangia na ataendelea kuchangia kiasi kwenye mpira wa miguu na mawazo yake na njia ya kufanya mambo,'' infantino aliiambia SKY Sport.
''Ni wazi kwamba, utampenda au kumchukia lakini mimi nitabaki nafasi ya kwanza. Tunahitaji watu kama yeye katika michezo, wazushi wote wanaosema na kufikiria si mara zote wana wasiwasi na diplomasia.
''Tunahitaji watu wa aina hii kwenye mpira na Mourinho ni mmoja wa watu hao, yeye ni shujaa kwenye soka.''
No comments:
Post a Comment