Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameonyesha nia ya kuimarisha kikosi chake kwenye usajili wa January kufuatia kuumia kwa Danny Ings ambaye atakuwa nje kutokana na majeraha ya goti.
Ings ambaye amefanyiwa oparesheni ya goti ambayo itamuweka nje muda mrefu, huku Klopp akitarajia kumkosa Sadio Mane mwakani kwasababu atakuwa kwenye majukumu ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Hali hiyo itampelekea Mjerumani huyo kufanya usajili ili kuweza kuziba pengo la wachezaji hao.
''Tunaangalia sokoni muda wote na bila shaka tunahitaji kujiandaa kwa hali yoyote na mojawapo mmoja wapo ni majeruhi,'' alisema Klopp akiwaambia UK Newspapers.
No comments:
Post a Comment