Nyota raia wa Ufaransa Dimitri Payet ameonyesha nia ya kuachana na West Ham dirisha dogo la usajili January mwakani huku mwenyewe akiweka wazi kuwa bado hajafunga mlango wa kuondoka Hammers. Payet ambaye alikuwa na kiwango kizuri kwa msimu wake wa kwanza akiwaeza kuwasaidia Hammers kuweza kumaliza nafasi ya saba na kusaidia timu yake ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2016 kufika fainali kwenye ardhi ya nyumbani.
West Ham ambayo inapigania kujiweka katika ubora wake toka wahamie uwanja wa London, wakishindwa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Europa na kushinda mechi tatu katika kumi na moja kwenye mechi za Premier League.
Na pengine hilo linamfanya Payet kuweza kutafuta timu atakayoweza kuhamia ili kulinda kipaji chake. Kwani kwenye kipindi cha Telefoot cha nchini Ufaransa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliulizwa swali kwamba kama ataweza kuhama West ham majira ya usajili mdogo hapo January, nae alijibu kwamba.
''Ninajiuliza mimi mwenyewe maswali mengine, nina matarajio, lakini sijafunga mlango kwa chochote,'' alisema.
''Siku zote miradi ya michezo inanivutia. Kwa sasa, PSG au Marseille hawajanifata wakiwa na lengo la kunitaka.
Na kwa upande wa Hammers ambao wameanza msimu 2016/2017 kwa kiwango kibaya Payet aliongezea kuwa ''ni mwanzo mbaya kwa West Ham, tunajaribu kuweza kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo.''
No comments:
Post a Comment