Monday, November 21, 2016

MURRAY ATHIBITISHA UBORA WAKE WA DUNIA.

Andy Murray akishangilia Ubingwa wa ATP 2016.
Muingereza Andy Murray amethibitisha ubora wake wa kuwa mchezaji namba bora duniani wa mchezo wa tenisi baada ya kumshinda Novak Djokovic na kufanikiwa kunyakua tuzo ya kwanza ya fainali za Dunia za ATP 2016.

Akiwa katika kiwango cha juu Mwishoni mwa mwaka, Murray ameshinda fainali hizo kwa 6-3 6-4 katika uwanja wa O2 arena mjini London
"Nina furaha kubwa sana kuwa mshindi, na kuwa namba moja duniani ni kitu cha kipekee sana". Alisema Murray.
Akiongeza kuwa ni nafasi ya kipekee sana kushindana na Novak katika mashindano kama haya.
Murray, mwenye umri wa miaka 29, amekuwa mchezaji bora katika mashindano 24.
Mashindano hayo pia yalimalizika kwa ushindi wa miaka minne wa Djokovic katika kinyan'ganyiro na Msebia huyo huku akimkaribia Roger Federer's.
Murray aliyeshinda vikombe 34 kwa mara kumi ameongeza " kabla ya hapa tumekuwa tukichuana katika fainali mbalimbali na katika Olimpiki lakini ninayo furaha kubwa kuwa mshindi.

No comments:

Post a Comment