Leo Ligi Kuu ya Hispania ijulikanayo kama LaLiga itasimamisha dunia kwa mechi kali na ya kusisimua baina ya miamba miwili mahasimu kwenye ligi hiyo kati ya Barcelona na Real Madrid kwenye mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Nou Camp Bracelona. Mchezo huo ambao mashabiki kutoka nchini Uingereza hawataweza kuuona kutokana na tofauti ya muda wa mchezo huo.
Madrid ikishuka dimbani kama kinara wa ligi hiyo ikifuatiwa na Barca kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo ambayo kila mmoja leo atahitaji kushinda ili ajitengenezee mazingira mazuri ya kuongoza ligi hiyo.

No comments:
Post a Comment