Saturday, November 5, 2016

KLOPP AGUSIA USAJILI JANUARY.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameonyesha nia ya kuimarisha kikosi chake kwenye usajili wa January kufuatia kuumia kwa Danny Ings ambaye atakuwa nje kutokana na majeraha ya goti.

LAKERS WAWATULIZA WARRIORS NBA


Golden State Wrriors wamepatwa na mshangao baada ya kukubali kipigo cha 117-97 kutoka kwa Los Angeles Lakers hapo jana kwenye muendelezo wa msimu mpya huku Antonio Spurs wakianza vizuri msimu mpya.

Friday, November 4, 2016

TOURE AOMBA MSAMAHA MAN CITY.


Hatimaye mchezaji raia wa Ivory Coast Yaya Toure anayechezea Manchester City ameweza kuomba msamaha kwa kocha wake Pep Guardiola ambaye kwa muda walikuwa hawana mawasiliano mazuri hali iliyopelekea wakala wa mchezji huyo kuingilia kati na kupelekea hali tete kwa kocha wa klabu hiyo.

Wednesday, November 2, 2016

MOURINHO APIGWA FAINI NA AFUNGIWA MECHI MOJA


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amefungiwa mechi moja baada  ya Jumamosi kutolewa nje kwenye mchezo wa Premier League waliotoka sare dhidi ya Burnley. Mourinho ambaye alitolewa nje kipindi cha pili kwenye mchezo huo uliochezwa Old Trafford baada ya kumtolea mwamuzi maneno machafu.

SIMBA SIYO YA MCHEZO, YANGA IKILALA SOKOINE 2-1.

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya leo hii pia kuendelelza rekodi yake ya kutopoteza mechi kwa kuifunga Stand United ya Shinyanga.

KUMI KUWANIA KOCHA BORA WA FIFA 2016.

Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) limeendelea na harakati zake za tuzo zake ambapo wametoa idadi ya makocha kumi kuwania nafasi ya kocha bora wa FIFA. Huku Ligi Kuu ya Hispania ikiongozwa na makocha Zinedine Zidane, Jose Enrique na Diego Simieno.

VPL-STAND KUMTULIZA SIMBA LEO.


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo kwa viwanja sita ambako kwa mara ya kwanza timu zote za Dar es Salaam zitakuwa mikoani kupambana kutafuta nafasi bora katika ligi hiyo iliyoanza Agosti 20, 2016 kabla kufifikia ukomo wa mzunguko wa 15, Novemba 12, mwaka huu.

UEFA MAMBO YANOGA: ARSENAL WAFUZU WAKITOKEA NYUMA.

 Group A



Klabu ya Arsenal hapo jana imeweza kufuzu raundi ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakitokea nyuma baada ya kuilaza Ludogorets Razgrad ya Bulgaria kwa mabao 3-2 mabao ya Xhaka , Groud na Ozil yaliweza kuifanya Arseanal kutinga 16 bora. Mesut Ozil alifunga bao la dakika za mwisho na kuwawezesha Arsenal kutoka nyuma 2-0 na kulaza Ludogorets Razgrad ya Bulgaria na kuwafikisha hatua ya mondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

MESSI AVUNJA REKODI YA RAUL, BARCELONA IKILALALA 3-1 KWA MAN CITY.

MSN wakishangilia bao.
Wakati mechi ikiendelea katika dimba la Etihad jijini Manchester Uingereza Lionel Messi anafunga bao ambalo linafanya avunje rekodi ya nyota Mhispania Raul Gonzalez kwenye Ligi ya Mabingwa. Raul ambaye kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa aliweza kufunga mara 53 kwa Real Madri na Schalke 04 katika magoli yake 71 kwenye miaka 16 idadi ambayo Messi ameifikia.

Tuesday, November 1, 2016

MURRAY AKARIBIA KUWA BINGWA NAMBA 1 WA TENNIS.


Mcheza tenisi raia wa Uingereza Andy Murray anakaribia kuwa mcheza tenisi namba moja duniani wa mchezo huo kama atafanikiwa kushinda taji la Paris Masters ambapo bingwa namba moja wa mchezo huo  Djokovic ameshindwa kutinga fainali.

MOURINHO AMRUDISHA SCHWEINSTEIGER KIKOSINI.


Mourinho na Bastian wakiwa mazoezini.
Kocha mtata wa Manchester United Jose Mourinho amemrudisha kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza cha Manchester United.
Kiungo huyo mwenye miaka 32 amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa chini ya umri wa miaka 23 tangu Jose Mourinho alipoteuliwa kuwa kocha msimu huu.

MASHABIKI WAPEWA NAFASI KUCHAGUA MSHINDI WA TUZO MPYA YA FIFA.



Ni kama vile tuzo ya Fifa Ballon d'OR imekufa baada ya France Football kuchukua umiliki wake kwenye tuzo hiyo, lakini FIFA ina mpango mpya kwa ajili ya kuwazawadia wachezaji bora kwa mwaka 2016. FIFA ilitangaza Jumatatu mpango wake mpya wa tuzo ujulikanao kama BEST FIFA FOOTBALL AWARDS ambao utafuata mchakato mbalimbali wa kupiga kura ukiwa tofauti kama mfumo wa awali wa upigaji kura ambapo mfumo watakaoutumia kwasasa ni pamoja na kura za mashabiki ikiwemo pia kura kutoka kwa manodha wa timu za taifa pamoja na makocha ambao asilimia 50 itatoka kwao kwa ajili ya mchakato wa uteuzi na asilimia 50 nyingine kutoka kwenye vyombo vya habari na kura za mashabiki za mitandaoni. Ambapo kura zilizopita zilikuwa zinatoka kwa manahodha, makocha na waandishi wa habari tu.

Monday, October 31, 2016

SARE ILINIFANYA NIWE NA CHIZI-POGBA

Kiungo wa Manchester united Paul Pogba ameweka wazi kwamba sare yao ya 0-0 dhidi ya Burnley ilimfanya ajisikie kupata uchizi, kwenye mchezo huo Man United walipata nafasi 37 za kushambulia goli la Burnley lakini walishindwa kuwafunga . Inakuwa mfulululizo wa sare kwa United kupata Old Trafold kwenye Premiere League.

USHINDI DHIDI YA WES BROM WAMPA KIBURI GUARDIOLA KUIVAA BARCELONA.


Kuelekea mechi yao ya marudiano dhidi ya  Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa, kocha Pep Guardiola amesisitiza kwamba mipango yake mikubwa zaidi iko kwa timu yake na sio wageni wao. Manchester City ambao walipoteza kwenye mchezo wao wa kwanza kwenye uwanja wa Nou Camp walilala 4-0 huku nyota Lionel Messi akifunga hat-trick kwenye ushindi hu, huku Pep akisisitiza kujiamini zaidi baada ya ushindi 4-0 waliopata dhidi ya West Brom Jumamosi iliyopita.

GRIEZMAN BADO ANA MATUMAINI YA KUSHINDA BALLON d'OR.

Mtu aliyevumbua kipaji cha mchezaji Antoine Griezmann amesema kwamba Mfaransa huyo bado ana matumaini ya kushinda Ballon d'OR, Eric Olhats ambaye alivumbua kipaji cha nyota huyo wa Atletico Madrid  akiwa na miaka 14 ambaye toka kipindi hiko alikuwa chini yake na akimuangalia alipokuwa Real Sociedad, hajakata tamaa ya kuwapiku nyota Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kutajwa kuwa mchezaji bora wa dunia.

BONAVENTURA AWAPA ZAWADI BAO LAKE WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI.

Mchezaji wa AC Milan Giacomo Bonaventura amewapa bao lake alilofunga kwa AC Milan 1-0 dhidi ya Pesara kwenye Serie A kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea katikati ya Italy. Mji wa Norcia uliweza kukumbwa na shambulio hilo lililokuwa na ukubwa wa 6.6 Jumapili.  Tetemeko hilo ambalo ni kubwa kuwahi kutokea nchini Italy toka mwaka 1980 limeharibu majengo mbalimbali , na watu takribani 20 wamejeruhiwa.

Sunday, October 30, 2016

GUARDIOLA ANALIPIZA KISASI KWA TOURE- WAKALA

Guardiola akitoa maelkezo kwa Yaya Toure.
Wakala wa mchezaji raia wa Ivory Coast Yaya Toure, Dimitri Seluk amesema kwamba meneja wa Manchester City Pep Guardiola analipa kisasi kwa Yaya kwa kumuweka nje ya kikosi chake. Kumekuwa na mgogoro unaoendelea kati ya wakala wa Yaya Toure na Pep Guardiola kufuatia wakala huyo kutoa maneneo ya hasira kwa kocha huyo wa City baada ya mchezaji kutocheza ndani ya kikosi hicho ambacho Yaya mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa mwezi Agosti kwenye mechi ya Klabu ya Mabingwa kati ya City dhidi ya Steau Bucharest.

YANGA DIMBANI LEO UHURU, MNYAMA ANA SPIDI YA 4G.


Ligi Kuu ya Vodacom  inaendelea leo kwa timu ya Yanga kuikaribisha Mbao FC kwenye uwanja wa Uhuru, Yanga ambayo itakuwa chini ya kocha wake Hans van Pluijm alierudi kuifundsha timu hiyo baada ya kujiuzulu nafasi ya ukocha baada ya uongozi wa klabu ya wanajangwani kumleta kocha mpya huku wakiwa na mkataba na Mholanzi huyo kitendo alichokiona amedharauliwa.

RAFINHA AIOKOA BARCELONA NOU CAMP KULALA KWA GRANADA.

Rafinha akishangilia bao lake dhidi ya Granada.
Barcelona iliweza kubakiza pointi tatu nyumbani kupitia bao la kipindi cha pili la dakika ya 48 kutoka kwa mchezaji wao Rafinha amabaye aliweza kuinusuru timu yakke kutoa sare kwenye Uwanja wa nyumbani wa Nou Camp. Granada ambayo katika mechi zake 22 zilizocheza Nou Camp imeweza kupoteza mechi zote hizo mbele ya Barcelona na kushindwa kufunga kwenye mechi zao nne za mwishoni.

HIGUAIN AIUA NAPOLI JUVENTUS STADIUM.

Gonzalo higuain akipongezwa na wachezaji wenzake.

Ilikuwa mechi ambayo ilivuta hisia za watu wengi kwenye ligi ya  Serie A nchini Italia kati ya ''kibibi kizee cha Tarino'' Juventus na Napoli na hisia hizo zilikuwa juu ya mchezaji Gonzalo Higuain aliyekuwa akichezea Napoli kabla ya kujiunga na Juventus kwa uhamisho wa euro million 90. Uhamisho ambao ulimfanya Higuain aonekane kama msaliti kwa kujiunga na Juventus ambao ni wapinzani wa Napoli ambapo alifunga mabao 36 kwa msimu uliopita. Mchezo huo ulimalizika kwa Juve kushinda 2-1 dhidi ya Napoli kwenye Uwanja wa Juventus.